Job 13


1 a“Macho yangu yameona hili lote,
masikio yangu yamesikia na kulielewa.

2 bHayo mnayoyajua mimi pia ninayajua;
mimi si mtu duni kuliko ninyi.

3 cLakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi
na kuhojiana shauri langu na Mungu.

4 dNinyi, hata hivyo, hunipakaza uongo;
ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote!

5 eLaiti wote mngenyamaza kimya!
Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima.

6 fSikieni sasa hoja yangu;
sikilizeni kusihi kwangu.

7 gJe, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu?
Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake?

8 hMtamwonyesha upendeleo?
Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake?

9 iJe, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi?
Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu?

10 jHakika angewakemea
kama mkiwapendelea watu kwa siri.

11 kJe, huo ukuu wake haungewatisha ninyi?
Je, hofu yake isingewaangukia ninyi?

12 lManeno yenu ni mithali za majivu;
utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi.


13 m“Nyamazeni kimya nipate kusema;
kisha na yanipate yatakayonipata.

14 nKwa nini nijiweke mwenyewe kwenye hatari
na kuyaweka maisha yangu mikononi mwangu?

15 oIngawa ataniua, bado nitamtumaini;
hakika nitazitetea njia zangu mbele zake.

16 pNaam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu,
kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu
atakayethubutu kuja mbele yake!

17 qSikilizeni maneno yangu kwa makini;
nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho.

18 rSasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu,
ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki.

19 sJe, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu?
Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife.


20 “Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili,
nami sitajificha uso wako:

21 tOndoa mkono wako uwe mbali nami,
nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu.

22 uNiite kwenye shauri nami nitajibu,
au niache niseme, nawe upate kujibu.

23 vNi makosa na dhambi ngapi nilizotenda?
Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.

24 wKwa nini kuuficha uso wako
na kunihesabu mimi kuwa adui yako?

25 xJe, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo?
Je, utayasaka makapi makavu?

26 yKwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu
na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu.

27 zUmeifunga miguu yangu kwenye pingu.
Unazichunga kwa makini njia zangu zote
kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu.


28 aa“Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza,
kama vazi lililoliwa na nondo.

Copyright information for SwhKC